المدة الزمنية 9:12

Njia Mbili rahisi za Kupata Mimba ya Mapacha kwa Mwanamke Yeyote | Mimba ya Mapacha.

بواسطة Dr. Mwanyika
15 315 مشاهدة
0
237
تم نشره في 2021/11/28

Jinsi ya kupata Mapacha Jinsi ya kupata Mimba ya Mapacha Mimba ya Mapacha Mapacha, Mapacha, Mapacha Endapo unahitaji kupata Mimba ya Mapacha na huna visababishi au vichochezi vya kupata Mimba ya Mapacha vilivyotajwa hapo chini Basi fanya Mambo haya mawili itaongeza uwezekano wa kupata Mimba ya Mapacha. Mambo hayo ni kama; 1. Tumia Dawa za Kuivisha Mayai kwenye Mifuko ya Mayai kama; Clomiphene citrate (Clomid) au Letrozole, Kwa kutumia Dawa hizi zinaweza kupelekea Mwanamke kutoa Mayai mawili kwa wakati mmoja wa mzunguko na kupata Mapacha wasio fanana endapo Mayai hayo yatarutubishwa na Mbegu Mbili tofauti za Mwanaume. Matumizi ya Clomiphene citrate huweza kusababisha kupata Mimba ya Mapacha kwa asilimia 5 Hadi 6 ukilinganisha na matumizi ya Gonadotropin ambazo huweza kupelekea Mwanamke kupata Mimba ya Mapacha kwa asilimia 20 hadi 40. 2. Mimba kutungwa Kwa usaidizi wa njia za kisayansi na teknolojia, ambapo Yai hutolewa kwenye Mfuko wa Mayai wa Mwanamke na kupandikizwa na Mbegu ya Kiume maabara na badae kijusi kilichoundwa kupandikizwa kwenye Mji wa Uzazi wa Mwanamke ambapo huweza pia kupandikizwa Vijusi viwili na kuongeza uwezekano wa kupata Mimba ya Mapacha. KUMBUKA; hasara ya njia hii huwa ni gharama kubwa zaidi lakini kuna uwezekano wa asilimia nyingi za kupata Mimba ya Mapacha Jinsi ya kupata Mapacha Jinsi ya kupata Mimba ya Mapacha Mimba ya Mapacha Mapacha, Mapacha, Mapacha ❤️Kisababishi kikubwa Cha Mimba ya Mapacha hakijulikani japokuwa kuna Baadhi ya Mambo yakiwepo huweza kuchochea Mwanamke kupata Mimba ya Mapacha. Mambo yanayoweza kuchochea Mwanamke kupata Mimba ya Mapacha ni Kama; 1. Uasilia, Tafiti zinaonesha kwamba Watu wa Africa hususani wanaishi kusini mwa Jangwa la Africa (Sub Saharan African) wanapata zaidi Mapacha ukilinganisha na Ukanda wowote ule katika Dunia, yaani wao Ni kwamba wanaweza kupata Mimba 5 za Mapacha kila Mimba 100. 2. Urithi, Mwanamke anayetoka kwenye Ukoo wenye Mapacha au hata Kama yeye mwenyewe ni Pacha ana anauwezekano mkubwa wa kupata Mapacha ukilinganisha na wengine ambapo anaweza kupata Mimba ya Mapacha 1 kwa kila Mimba 60. 3. Ulaji wa Viazi pori au Magimbi huweza kuongeza uwezekano wa kupata Mapacha kwa sababu huwa na phytoestrogen nyingi ambazo huweza kupelekea Mwanamke kupata Mimba ya Mapacha. 4. Mwanamke anayebeba Mimba katika Umri mkubwa Kati ya Miaka 30 hadi 35 ana uwezekano mkubwa wa kupata Mimba ya Mapacha kwa sababu anaweza kutoa Mayai mawili katika Mzunguko mmoja wa Hedhi. 5. Mwanamke mwenye Uzito mkubwa na mrefu zaidi (BMI = 30kg/M²) anauwezekano mkubwa wa kupata Mimba ya Mapacha ukilinganisha na Mwanamke mwenye umbile Dogo. 6. Matumizi ya Maziwa ya Ng'ombe kwa wingi, huweza kupelekea Mwanamke kupata Mimba ya Mapacha ingawa Kuna Baadhi ya tafiti zimekanusha uthibitisho huu. 7. Matumizi ya folic acid hayawezi kuongeza uwezekano wa kupata Mapacha japokuwa Kuna Baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba Mwanamke anayetumia Folic acid anaweza kupata Mimba ya Mapacha. Jinsi ya kupata Mapacha Jinsi ya kupata Mimba ya Mapacha Mimba ya Mapacha Mapacha, Mapacha, Mapacha Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp ©Dr.Mwanyika #drmwanyika #mamaafya #PataMapacha

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 173