المدة الزمنية 7:8

Je unaweza kupata Hedhi ktk Ujauzito | Je Kwa nini unatokwa na Damu Ukeni ktk kipindi cha Ujauzito

بواسطة Dr. Mwanyika
21 377 مشاهدة
0
216
تم نشره في 2021/11/07

Je ni kweli kwamba unaweza kupata Hedhi katika kipindi cha Ujauzito? Hapana! Ukweli ni kwamba mara baada ya kupata Ujauzito au Mimba huwezi kupata Hedhi, Baadhi ya Wajawazito hususani wale ambao hupata Mimba kwa Mara ya Kwanza (Prime gravida) huweza kuchanganya wanapotokwa na Damu mwanzoni mwa Ujauzito na Hedhi yao! Tafiti zinaonesha kwamba asilimia 10 mpaka 15 ya Wajawazito huweza kupata Dalili za kutokwa na Damu katika Ujauzito wao hususani Mimba inapokuwa chini ya wiki 16 au chini ya Miezi 4 ya Ujauzito. Kutokwa na Damu katika kipindi cha Ujauzito huweza kuhatarisha Mimba yako na matokeo yafuatayo mfano; 1. Mimba Kutoka au kuharibika na hivyo kutojifungua Mtoto wako. 2. Kujifungua Mtoto kabla ya wakati. 3. Kujifungua Mtoto mwenye Uzito wa chini zaidi. 4. Kupungukiwa Damu ktk kipindi cha Ujauzito au hata baada ya kujifungua au Mimba yako kuharibika. MAMBO YANAYOPELEKEA MJAMZITO KUTOKWA NA DAMU. 1.Mimba kutishia kutoka au kuharibika kabla ya kujifungua! 2. Kondo la Nyuma linapojishikiza kwenye Mji wa Uzazi huweza kupelekea kutokwa Damu katika kipindi Cha Ujauzito hususani mwanzoni mwa Ujauzito ambapo hutokea katika siku zile zile ambazo Hedhi ya kawaida ingetokea japokuwa huwa kunakuwa na utofauti na Hedhi ya kawaida Damu hutoka kidogo na kwa siku chache na badae hukata yenyewe. 3. Mimba kutunga nje ya Mji wa Uzazi huweza kupelekea kutokwa na Damu ktk cha kipindi Cha Ujauzito (Arias Stella Reaction) hususani mwanzoni mwa Ujauzito chini ya wiki 12 za Ujauzito kutoka na Upungufu au uzalishwaji mdogo wa Homoni ya Progesterone ukilinganisha na Mimba ya kawaida. 4. Mimba Zabibu, Mimba Zabibu kwa kawaida huwa lazima iharibike au itoke baada ya muda fulani wa Ujauzito hususani mwanzoni mwa Ujauzito (Chini ya wiki 16) hivyo huwesa kupelekea kutokwa na Damu katika kipindi cha Ujauzito. 5. Sababu zisizo Julikana, kuna baadhi ya Wajawazito hutokwa na Damu bila kuwa na sababu zinazojulikana au zinazopelekea kutokwa Damu katika kipindi cha Ujauzito. KUMBUKA: Asilimia nyingi ya Wanawake wanaotokwa na Damu katika kipindi cha Ujauzito hujifungua Salama Watoto wao. Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp ©Dr.Mwanyika #drmwanyika #mamaafya # HedhiKtkUjauzito

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 231