المدة الزمنية 6:37

Kukojoa Mara kwa Mara kwa Mjamzito | Sababu za Kukojoa Mara kwa Mara ktk kipindi cha Ujauzito

بواسطة Dr. Mwanyika
13 087 مشاهدة
0
138
تم نشره في 2021/12/23

Kukojoa Mara kwa Mara kwa Mjamzito huweza kusababishwa na Visababishi Kama; A. MABADILIKO YA KAWAIDA KTK KIPINDI CHA UJAUZITO./PHYSIOLOGICAL CHANGES OF PREGNANCY. Kwa sababu ya mabadiliko ya kifiziolojia ya kawaida ya Mwili wa Mjamzito katika kipindi cha Ujauzito huweza kupelekea Mjamzito kukojoa Mara kwa Mara kutokana na sababu zifuatazo. 1. Ongezeko la Damu ktk Kipindi Cha Ujauzito. Mabadiliko haya katika kipindi cha Ujauzito hutokana na maongezeko ya nahitaji ya Mwili wa Mjamzito Pamoja na Mtoto anayetengenezwa Tumboni mwa Mjamzito, hupelekea Damu nyingi kwenda kwenye Figo na kutengeneza Mkojo mwingi ukilinganisha na Mwanamke asiyekuwa Mjamzito! 2. Mabadiliko ya Homoni na Ongezeko kubwa la Homoni ya Progesterone na HCG kwa Mjamzito ambayo hulegeza Baadhi ya nyuzi mfano; ligamenti ambazo hudhibiti utolewaji wa Mkojo katika Kibofu Cha Mkojo na Mrija wa Mkojo(Urethra) matokeo yake Mjamzito anashindwa kuzuia na kubaki na Mkojo kwa Muda mrefu hata kwa Ujazo Mdogo wa Mkojo hivyo hutakiwa kwenda kukojoa Mapema. 3. Ukuaji wa mfuko wa Uzazi. Mimba inapofikisha Wiki 10 hadi 12 au Miezi Mitatu ya mwanzoni mwa Ujauzito, Mara nyingi mfuko wa Uzazi huwa kwenye sehemu ya juu ya Kinena nyuma ya Kibofu Cha Mkojo hivyo hupelekea kubanwa kwa Kibofu Cha Mkojo Kati ya Mfuko wa Uzazi na Mfupa wa Kinena na kupelekea kupunguza kwa Ujazo wa Kibofu Cha Mkojo hivyo hupelekea Kibofu kujaa mapema na Mjamzito hukojoa Mara kwa Mara. Miezi Mitatu ya katikati Mara nyingi mfuko wa Uzazi unakuwa juu zaidi hivyo hali ya kubanwa kwa Kibofu Cha Mkojo hupungua na Mjamzito hupunguza kukojoa Mara kwa Mara katika kipindi Cha Kati Cha Ujauzito Miezi 4 Hadi Miezi 6 ya Ujauzito. Miezi Mitatu ya Mwishoni mwa Ujauzito Kutokana na Mtoto kushuka Mjamzito anapojiandaa kujifungua au Mtoto anapojiandaa kutoka basi kunakuwa na uwezekano wa Kichwa au Kiungo chochote Cha Mtoto kubana Kibofu Cha Mkojo kuelekea kwenye Mfupa wa Kinena, hivyo hupelekea Mjamzito kukojoa Mara kwa Mara pia. B. Magonjwa/ Maambukizi ya Vijidudu kwenye mfumo wa Mkojo /Urinary Tract Infection/UTI. Endapo Mjamzito unakojoa mara kwa mara, Unapata maumivu wakati wa kukojoa, Unapata maumivu ya Tumbo Chini ya Kitovu, Homa, Maumivu pembeni mwa Tumbo na nk inawezekana una Maambukizi ya Bacteria kwenye mfumo wa Mkojo hii ni Kutokana na maongezeko ya homoni za Progesterone katika kipindi cha Ujauzito, hupelekea kupungua kwa mjongeo wa Mkojo kwenye Mirija ya Mkojo na kupelekea Mkojo kubaki kwa muda mrefu kwenye mfumo wa Mkojo na kupelekea Bakteria kuzaliana na kusababisha Ugonjwa kwenye mfumo huo/UTI. Hata hivyo siyo Mara zote Mjamzito anaweza kuwa na Dalili endapo ana Vijidudu kwenye mfumo wa Mkojo Hali hii huitwa Asymptomatic Bacteuria, Aina hii ya shida huweza kugunduliwa endapo Mjamzito amefanya kipimo Cha Mkojo (Urinalysis) na hana Dalili zozote za UTI. Hivyo ni vema kufanya kipimo Cha Mkojo Cha UTI hata kama inawezekana visababishi vya kukojoa Mara kwa Mara ni Mabadiliko ya kawaida kwa Mjamzito katika kipindi cha Ujauzito. NB: ENDAPO UNA UTI UNAHITAJI KUANDIKIWA DAWA NA DAKTARI. Nifuatilie kwenye channel yangu kuhusu Mambo ya Ujauzito. /c/DrMwanyika Nifuatilie Instagram kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.instagram.com/dr._mwanyika/ Nifuatilie kwenye website hii kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://mamaafya.com/ Nifuatilie kwenye Facebook page kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://www.facebook.com/JapideAfya/ Usisahau kudownload app ya Mama Afya Bora kwa ajili ya Mambo ya Ujauzito. https://play.google.com/store/apps/details?id=com.wapnum.mamaafyaapp #Kukojoakojoa #DrMwanyika #MamaAfya

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 138