المدة الزمنية 11:56

Kilio cha mda Mrefu cha Barabara sasa bas Naibu Naziri Ujenzi na Uchukuzi GODFREY KASEKENYA

بواسطة DSS TANZANIA
249 مشاهدة
0
2
تم نشره في 2021/12/02

Kilio cha mda mrefu cha barabara kwa wanakijiji wa Ndola,Ishinga ,Shuba na Ibaba vilivyopo Ileje mkoani Songwe kinaenda kuisha baada ya serikali kutoa kiasi cha shilingi milioni 243.01 kwa ajiri ya kutengeneza barabara yenye urefu wa kilometa 21 itakayo pita katika vijiji hivyo. Akithibitisha hayo Mbunge wa jimbo la Ileje Godfrey Kasekenya alipo tembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inaenda kutatua changamoto ya barabara katika vijiji hivyo . Afsa wa TARURA akizungumza kwa niaba ya Meneja wa TARURA wilaya ya Ileje amesema kuwa mradi huo wa barabara hadi sasa umekamilika kwa Asilimia 60 na wanatarajia utakamilika 23 Febuari 2022. Huku Mwahandisi wa mradi bwana Mathaw Mbaluku amesema kuwa kazi inaendelea vizuri japo anakutana na changamoto ya uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo, ambapo inawalazimu kuchukua maji vijiji jirani na eneo hilo ,huku akiahidi kumaliza kazi hiyo kwa muda alio pangiwa. Lakini pia wananchi wa vijiji ambavyo vitanufaika na barabara hiyo wamesema kuwa kumaridhika kwa barabara hiyo kwao ni ukombozi mkubwa kiuchumi kwa sababu walikuwa wanaangaika katika kusafirisha mazao yao kama kahawa ,ndizi na vyungu vya kufinyanga ambapo walikuwa wakiwatumia vibarua kubeba mazao yao umbali mrefu hivyo kupelekea kuwa na kipato kidogo.dsshabari #dss #kigoma #kimkardashian #kigomaujiji #bigsundaylive #mwanza #mwanzamwanza #dsstv #ileje #yatima #ilejefm #wasafimedia #wasafifm #dss #kigoma #kimkardashian #kigomaujiji #bigsundaylive

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0