المدة الزمنية 8:2

WALIOONDOLEWA NA VYETI FEKI WAPEWE HAKI ZAO-MBUNGE MRISHO GAMBO

بواسطة Millard Ayo
14 949 مشاهدة
0
65
تم نشره في 2021/04/24

Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo ameitaka Serikali kuwaangalia watumishi wa umma waliofukuzwa kazi kwa vyeti feki kwa kuwapa mafao na kiinua mgongo chao. Mbunge huyo ametoa ombi leo Ijumaa Aprili 23, 2021 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mwaka 2021/2022 Gambo amesema Serikali ilifanya zoezi muhimu na nyeti la kufanya uhakiki vyeti vya watumishi wa umma na liliwasaidia kufanya usafi kwenye sekta ya utumishi wa umma kwa kuwaondoa wasiostahili lakini haikuwalipa stahiki zao. Amesema anakumbuka kuwa taarifa ya mwisho ya Serikali ilisema 511589 ambao ni sawa na asilimia 96.71 walihakikiwa lakini 14,409 walibainika kuwa na vyeti feki na watumishi 1907 walikuwa bado hawajapeleka uthibitisho wa vyeti vyao kwa ajili ya kuhakikiwa.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 84