المدة الزمنية 1:27:6

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA EVENING GLORY

7 914 مشاهدة
0
149
تم نشره في 2021/03/11

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA EVENING GLORY 11/3/2021 UJUMBE WA LEO: "NJIA YAKO DUNIANI" "YOUR WAY UPON THE EARTH" NAMNA ROHO ZA WATESI ZINAVYOWEZA KUHARIBU NJIA YAKO DUNIANI Matendo 12 : 1 - 5 Mhubiri 1 : 1 - 8 Waefeso 6 : 10 - 18 Zaburi 71 : 10 - 13 Luka 19 : 41 - 44 Luka 21 : 34 - 36 Matendo 12 : 1 - 5 1 Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa. 2 Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga. 3 Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa. 4 Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu. 5 Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. Mhubiri 1 : 1 - 8 1 Maneno ya Mhubiria, mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu 2 Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. 3 Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua? 4 Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. 5 Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. 6 Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake. 7 Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena. 8 Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia. Waefeso 6 : 10 - 18 10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; Zaburi 71 : 10 - 13 10 Kwa maana adui zangu wananiamba, Nao wanaoniotea roho yangu hushauriana. 11 Wakisema, Mungu amemwacha, Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya. 12 Ee Mungu, usiwe mbali nami; Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia. 13 Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya. 41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako. Luka 21 : 34 - 36 34 Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; 35 kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima. 36 Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu. Mhubiri : Mwl. Emilian Katubayemo Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 5