المدة الزمنية 7:36

WOKOVU WETU UPO KARIBU KULIKO TULIPOANZA KUAMINI warumi 13:11

بواسطة SIRI ZA BIBLIA
1 626 مشاهدة
0
39
تم نشره في 2021/07/10

#dhambi#msalaba#wokovu#yesu Maandiko yanasema kuwa hiki ni kipindi cha rehema. Kipindi ambacho Yesu bado anafanya kazi ya kuwapatanisha wanadamu na Mungu wao. Nataka nikwambie mpendwa kuwa, kulingana na maandiko, kipindi hiki hakitaendelea milele zote. Maandiko yanasema kuwa, hivi karibuni Mungu atafunga huduma hii ya kusamehe dhambi. Akifunga huduma hii Yesu atasema "imekwisha, mwenye dhambi na aendelee kuwa na dhambi zake" (Ufunuo 22:11). Wakati huo wale wote ambao hawatakuwa wamesalimisha maisha yao, ambao hawatakuwa wametubu na kuacha dhambi haitawezekana tena kabisa kusamehewa dhambi zao. Hakika wataangamia milele zote katika uovu wao kwa sababu hawakutaka kuuacha. Hiki ni kipindi ambacho Mungu anaendelea kutoa wito kwa wote wenye mwili, anawasihi sana sana waache dhambi zao wasahihishe njia zao zilizopinda wapate kuokolewa. Hatujui ni lini rehema hizi zitakoma lakini pia hatujui maisha yetu yatakoma lini. Tunapaswa kujipatanisha na Mungu wetu wakati wote. Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu uko karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini "Warumi 13:11" Maarifa ya Ki-Mungu @SIRI ZA BIBLIA www.sirizabiblia.com +255 758 708 804 https://linktr.ee/sirizabiblia Instagram Account https://www.instagram.com/siri_za_biblia/

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 14