Samia Suluhu Hassan, Rais - Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Vyombo vya Habari vina mchango mkubwa kulinda Umoja wa Kitaifa, Usalama Nchi, Kuchochea shughuli za maendeleo. Vinasaidia Kufichua Maovu kwenye Jamii ikiwemo uzembe kazini, rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma
Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa nchi yetu
i. Vyombo vya habari kunyimwa matangazo
Hili la Vyombo vya Habari kunyimwa matangazo, sijalikuta mezani kwangu
Kuna ushindani katika kupata matangazo
Kule Zanzibar tunayo Suluhu Network TV, mpaka leo mishahara tunachanga! Hatujapata matangazo ya kuendesha kituo
ii. Madeni
Suala la Madeni, nitashirikiana na Waziri Mkuu yalipwe kidogokidogo. Lakini lazima tuyahakiki kama ni madeni halali
iii. Stimulus package
Stimulus package kwaajili ya athari za #COVID19 kwakweli ni changamoto
Tunaweza kuliangalia huko mbeleni, hata Uchumi wenyewe wa Taifa unapitia wakati mgumu
iv. Leseni kulipiwa kwa Dola
Suala la Leseni kulipwa kwa Dola hata nami naliona kuwa ni changamoto. Hatuwezi kuwa Watumwa wa Sheria tunazozitunga. Tutakaa kitako tuangalie tunakwendaje
v. Kazi ya Urais
Kazi ya Urais ni ngumu, lakini urais ni Taasisi
Rais hafanyi kazi peke yake; ndani ya Ofisi yake kuna Wasaidizi kadhaa lakini si rahisi kihivyo. Inabidi ujue kila kitu kinachotokea, usome na utafute
Inakuwa ngumu zaidi kama hukujipanga kuichukua
vi. Siku 100 Madarakani
Katika siku 100 nilizokaa madarakani, kuna ambayo nami nimesikia yamefanyika nami nikashangaa
Tumehimili vishindo; thamani ya pesa yetu bado iko imara na mfumuko wa bei umedhibitika
Tuna akiba ya takribani Dola Bilioni 4.97 hivyo uhakika wa kujiendesha miezi 6 upo
vii. Idara ya Habari kwenda Wizara ya Teknolojia ya Habari
Kuhusu pendekezo la Idara ya Habari iende kwenye Wizara ya Teknolojia ya Habari, tutakaa tuyaangalie kwa pamoja
Tukiwa na 'justification' ya kutosha basi tunaweza tukaamua vinginevyo
viii. Kukabiliana na Covid 19
Kuna wanaoona hatuko serious ktk mapambano dhidi ya Covid 19
Nilipoingia madarakani nilitamani tupambane na ugonjwa huu kama wanavyofanya mataifa mengine
Tanzania tuna wagonjwa zaidi ya 100 wenye wimbi la tatu la Covid 19
Tumeamua tukubali chanjo kwa walio tayari
Tanzania tumeingia kwenye COVAX community
Wataalamu wetu wanafanyia kazi Chanjo ipi inafaa kwa Watanzania
Kuna mashirika mengi wamejitokeza kutaka kusaidia Watanzania lakini lazima wataalamu wetu ndio watoe ushauri kitaalamu
Mapambano ya Covid 19 si ya Serikali tu. Sisi kama Serikali tunahimiza yale yanayoshauriwa na wataalamu; kama unaamini kwenye kupiga nyungu - wewe piga. Kila mmoja atekeleze wajibu wake. Jikingeni sana na wakingeni watoto
Tuna $470m za kuagiza chanjo na vifaa vya kupambana na Covid 19
ix. Teuzi za viongozi
Kwenye teuzi hatuwezi kumchukua kila aliyesema “CCM OYEE”
Kwenye teuzi kuna waliokuwa wapinzani, kuna wasiokuwa na vyama na hata wana CCM. None is left behind
x. Uwekezaji nchini
Wawekezaji waliosajiliwa kuanzia Machi hadi Mei ni mara mbili ya waliojitokeza kipindi kama hiki mwaka jana
Naendelea kufungua milango ya kukuza uchumi
xi. Katiba Mpya
Naomba nipeni muda kwanza niisimamishe nchi kiuchumi halafu tutashughulikia mengine
Tutashughulikia Katiba Mpya lakini Vyama vya Siasa viendelee kufanya Siasa kwenye maeneo yao
Sisemi Katiba sio ya maana, ni ya maana sana