المدة الزمنية 25:5

Bunge la Ulaya (EU) lajadili hali ya kisisasa Tanzania na kukamatwa kwa Freeman Mbowe

بواسطة JamiiForums
5 918 مشاهدة
0
55
تم نشره في 2021/12/02

Mwenyekiti wa kamati wa mambo ya nje kwenye Bunge la Ulaya, David James McAllister amesema anawasiliana na watu wengi nchini Tanzania ambapo amesema wapo kwenye hali ambayo viongozi, wanachama na wafuasi wa upinzani wanakumbana na udhalilishaji, kushikiliwa kinyume cha sheria na vitisho. Kwa upande wake mkurugenzi wa mambo ya Afrika kutoka umoja wa Ulaya, Laranjinha Rita amesema kuna sababu za matumaini Tanzania ambapo miezi ya karibuni kumekuwa na mwanzo mzuri kwa Rais Samia nyumbani na kimataifa ambapo ametambulisha baadhi ya mabadiliko. Laranjinha amemueleza Rais Samia kwenye uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya habari na mabadiliko hayo yamepokelewa vizuri na jamii ya kimataifa. Pia ameongelea ruhusa ya kurudi shuleni kwa wanafunzi waliopata ujauzito. Laranjinha amesema pamoja na hatua zilizofikiwa kuna mapungufu machache ikiwemo demokrasia ya vyama vingi ambapo hakuna uwakilishi wa upinzani kwenye bunge, mwenyekiti wa chama cha upinzani kushikiliwa na umoja wa ulaya itaendelea kufatilia kwa karibu.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 18