المدة الزمنية 11:6

Akina ZITTO watoa tamko zito baada ya Polisi kumkamata Askofu anayemuunga mkono Tundu Lissu

بواسطة Gilly Bonny Tv
35 539 مشاهدة
0
89
تم نشره في 2021/02/16

JANA Tarehe 15/2/2021 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam lilitoa taarifa ya kumkamata Askofu mwamakula kwa madai ya tuhuma ya kosa la kuhamasisha Maandamano nchi nzima kwa lengo la kudai kupatikana kwa Katiba Mpya nchini. ACT-Wazalendo inalaani na kupinga kitendo hicho cha Jeshi la Polisi kumkamata Kiongozi wa kiroho na Kijamii aliyejitolea kuhamasisha kwa njia za amani uwepo wa Mabadiliko ya Katiba ya Nchi itakayotoa fursa ya kuwa na TUME HURU YA UCHAGUZI. 1. Askofu Mwamakula amehamasisha kufanya “MATEMBEZI YA HIARI” ambayo ni haki yake ya Kikatiba kama Mtanzania, Jeshi la Polisi halijaeleza ni Sheria ipi imevunjwa kwa kuandaa matembezi ya Hiari? Katiba ya Nchi Ibara ya 20(1) inaeleza kuwa; “Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani,…”

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 118