المدة الزمنية 35:7

Salama Na Gabo Ep 25 | MTOGAPAAFWE Part 1

بواسطة YahStoneTown
127 629 مشاهدة
0
1.5 K
تم نشره في 2020/07/19

#YAHStoneTown #SalamaNa #PodCast SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm� �� ‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru� �� GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Jina halisi ni Salim Ahmed Issa, na kwa mujibu wa niloyasoma ni mjukuu wa moja ya watu maarufu mkoani Iringa ambaye alikua anatambulika kama Mtogapaafwe Kiyeyeu. Huyo alikua ni BABU wa Gabo Zigamba kabisaa ambaye binti yake Rafia Issa Kiyeyeu ndo Mama mzazi wa Gabo huyu tunayemfahamu mimi na wewe. Unaambiwa kaburi la Marehemu Mzee Mtogapaafwe lilikua na maajabu sana, ila hiyo ni khadithi ya siku nyengine. Hapa ilikua juu ya utambulisho wetu kwake na sifa zake actor hodari toka kwetu Tanzania. Gabo si moja ya marafiki zangu ila baada ya kuonana hapa ndo urafiki wetu ulipoanzia baada ya kujua pia tunafanana kwa mambo mengi kwa kweli. Gabo ni MTENDAJI, kuongea anaongea pale anapokua huru na mazingira ila mara nyingi huwa hasemi sana bali anatenda zaidi. Toka nimemsikia mara ya kwanza mwaka 2016, kijana huyu amekua akishinda tuzo mbali mbali na kutengeneza base yake vizuri kabisa. Na ukimuuliza mtu yoyote anayefuatilia mambo ya filamu kuhusu yeye basi hakika utaskia kipaji chake kikizungumziwa pia. Tuzo mbali mbali Gabo ameziokota sana na mpaka kuna kipindi ilikua inasemekana kwamba yeye ndo ‘mrithi’ wa Marehemu Steven Kanumba kitu ambacho kinaweza ikawa motivation au viatu vikubwa sana kwa miguu yake. Swali ni je, anajua watu wanamuona huko? Kwenye kikao chetu zaidi mimi nilitaka kumfahamu haswa, kumfahamu yeye binafsi na familia yake, nilitaka kufahamu kinachompa raha na karaha. Nilitaka kujua alianzia wapi, nilitaka kujua starehe yake, mipango yake, mitihani yake. Nilitaka kujua kuhusu jina lake, kuhusu kipaji chake, kuhusu dini na mahusiano. Kuhusu industry na ushindani wa ndani na nje na Sanaa kwa ujumla. Na nashkuru alinipa time yake na yangu matumaini humu utapata chochote kitu cha kukufunza jambo. Tafadhali enjoy. Love, Salama. Soundtrack Yeah by @MarcoChali /watch/QLnf4BH1euC1f Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 227