المدة الزمنية 15:32

Aina Mbili Za Madeni Na Madeni Ya Kuepuka Kwenye Maisha Yako

بواسطة Dr. Makirita Amani
10 436 مشاهدة
0
113
تم نشره في 2017/08/07

Habari za leo rafiki yangu? Hakuna kitu kimekuwa mzigo kwa wengi na kuwazuia kufanikiwa kama mikopo na madeni. Japo wengi wamekuwa wakidanganyika mikopo ina manufaa kwao, wengi wamekuwa wanauona ukweli halisi wa mikopo pale wanapoichukua. Sasa changamoto kubwa sana kwenye madeni ni kwamba, watu wanadanganywa sana. Wamekuwa wanadanganywa na kauli kuu mbili; Kauli ya kwanza ni kwamba huwezi kufanikiwa bila ya kukopa, au matajiri wengi wanakopa na ndiyo maana wamefikia utajiri. Kauli ya pili ni ile kwamba mtu anakopesheka. Hili ni kauli mbili ambazo zimewapoteza wengi, kwa kuwaingiza kwenye madeni ambayo hayana msaada kwao na kuishia kuteseka. Kwenye kipindi chetu cha ONGEA NA COACH leo nimezungumzia na kuchambua aina kuu mbili za madeni ambazo unapaswa kuzijua kabla hujaingia kwenye madeni. Pia nimekushirikisha madeni gani uyaepuke sana kwenye maisha yako, na madeni yapi ambayo yana msaada kwako. Kabla hata hujaanza kukadiria ni madeni gani mazuri kwako, nikuambie tu, madeni unayofikiria kwako ni mazuri ni mabaya mno. Kwa mfano, kuchukua mkopo wa kujenga nyumba, kununua gari au hata kuanza biashara, ni madeni mabaya kwako na yatakurudisha nyuma. Kabla hujaanza kubisha hili, nakusihi uangalie kipindi hichi cha leo, ili uweze kupata maarifa sahihi na kuweza kuchukua hatua sahihi.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 24