المدة الزمنية 4:6

Hii ndio vita iliyochukua muda mfupi zaidi na yenye matokeo ya kustajabisha

بواسطة Radio Mbiu
5 344 مشاهدة
0
27
تم نشره في 2019/02/26

VITA YA SIKU SITA Hii ni vita iliyovunja rekodi ya dunia kwa kutumia muda mfupi ikiwa na matokeo ya kustaajabisha. Ilikuwa ni kati ya #Israeli na mataifa yote ya kiarabu, yakiongozwa na Misri, yakisaidiwa na Urusi. Wakiwa na lengo la kuifuta Israeli kwenye ramani ya dunia, Misri, Jordan, Syria na Iraq, waliweka tayari kikosi cha wanajeshi wapatao 465,000 vifaru 2,800 na ndege 800. Hivi vyote tar 15/05/1967, vilishaletwa mipakani mwa Israeli. UN iliweka askari wa kulinda amani Israeli tangu 1956, lakini GAMAL ABEL NASSER raisi wa Misri aliwaamuru kuondoka kwa usalama wao, wakakimbia. Tarehe ilokuwa imepangwa kufuta Israel ni 05, June 1967. Siku hiyo LEVI ESHKOL, waziri mkuu wa Israeli aliamuru mashambulizi. Saa 1:14 asbh wakati marubani wa Misri wakinywa chai, ghafla ndege za Israeli zilianza mashambulizi. Ndani ya nusu saa, ndege 300 za misri zilishateketezwa. Hadi jioni siku ya kwanza, ndege zote za Misri na Jordani zilishaharibiwa! Hadi siku ya tatu, raisi wa Misri aliomba UN ije kuwaokoa! MATOKEO YA VITA: Kwa Israeli, wanajeshi 776 na raia 20 waliuawa na waliojeruhiwa ni 4,517. Wanajeshi wa Misri waliouawa ni zaidi ya 15,000. Wajordani waliouawa ni 6,000 na Wasyria 2,500 na Wairaq 10. Jumla ya Wanajeshi waarabu waliouawa ni zaidi ya 23,510. Ndege 452 zikiwemo zote za Misri ziliharibiwa kabisa. Mamia ya vifaru viliteketezwa, na maelfu ya wanajeshi walitekwa na Israeli. Ndege za Israeli zilizoharibiwa ni 46, kati ya 260 walizokuwa nazo.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 4