المدة الزمنية 19:21

Wimbo Wangu 13 | | Dr. Jacob Kihila

بواسطة Mwenge SDA Church
172 مشاهدة
0
2
تم نشره في 2021/04/22

Wimbo Wangu ni kipindi maalumu cha kujifunza namna sahihi ya uimbaji wa Nyimbo za Kristo. Kipindi hiki kinarushwa mbashara (live), kila siku ya Alhamisi, kuanzia saa 12:00​ jioni. Katika kipindi hiki msikilizaji pia atapata fursa ya kujifunza teolojia (fundisho la kiroho) katika wimbo husika na historia na mazingira ya uandikwaji wake. Kipindi hiki kinasimamiwa na wakufunzi mahiri wa muziki wa ibada na wanyenyekevu wanaojifunza Neno la Mungu. Uimbaji ni Ibada, karibu kuungana na wakufunzi hawa kujifunza namna nzuri zaidi ya kumuabudu MUNGU wetu. Kipindi cha leo kinachambua Nyimbo mbili ambazo ni; 1. "Jaza Kikombe Changu" (Wimbo namba 287) na "Mungu Anakujali" (Wimbo namba 35), zote zikipatikana katika kitabu kikubwa cha Nyimbo za Kristo. Karibu kutuma mapendekezo ya wimbo wakujifunza kipindi kijacho kupitia barua pepe: live@mwengesdachurch.or.tz au ujumbe wa simu kwa namba: +255 752 599 733 Barikiwa! Ukiwa na swali, uhitaji wa maombi, ubatizo wasiliana na Mchungaji kwa namba +255 677 048 069 au +255 784 458 957. Kama una ushauri usisite kutuma kwa namba +255 713 343 939 au barua pepe live@mwengesdachurch.or.tz. Tunapenda kukujulisha kupitia channel hii, kuna vipindi mubashara mbalimbali kila siku jioni kama; Ongeza Ujuzi, Afya ni Mtaji, Kona ya Watoto, Lijue Kanisa na Ibada mbalimbali na maombi. Karibu ku-SUBSCRIBE ili uwe sehemu ya wengi wanaobarikiwa: https://bit.ly/SUBSCRIBE-Now, watumie na marafiki pia. Karibu pia kutembelea tovuti yetu: www.mwengesdachurch.or.tz Mungu akubariki.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0