المدة الزمنية 6:46

CCM: Lazima kuwepo na muda wa kazi na muda wa siasa.

بواسطة The Chanzo
77 مشاهدة
0
1
تم نشره في 2021/12/08

Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amezungumza na vyombo vya habari Ofisi ndogo ya CCM ya makao makuu iliyopo mtaa wa Lumumba kuelezea mambo mbalimbali kuelekea maazimisho ya miaka sitini ya Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika sasa Tanzania bara. Katika mkutano huo, Chongolo amesemaa kwamba huu ni wakati chama kilichopewa dhamana ya kuongoza dola kutekeleza mambo yale ambayo ilihaidi, hivyo vyama shindani ambavyo havikupewa hiyo ridhaa viache kufanya shughuli za kisiasa hadi pale wakati wa uchaguzi mkuu ili viwaeleze wananchi kama kuna mahali chama tawala kimekosea. Pamoja na hilo, pia amezungumzia wajibu wa chama chake CCM katika kulinda uhuru ambao Disemba 9, 2021 itatimia miaka sitini ya Uhuru wa Tanganyika tangu ulipotwaliwa toka kwa Wakoloni Disemba 9, 1961.

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 0