المدة الزمنية 52:39

MALANGO YA NDOTO YANAVYOTUMIKA NA ADUI (II) - PASTOR SUNBELLA KYANDO

22 742 مشاهدة
0
289
تم نشره في 2021/07/08

Mathayo 13:24-26 [24]Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; [25]lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. [26]Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. Mpanzi alienda kupanda mbegu lakini adui alisubiri wakati wa usiku naye akaenda kupanda uharibifu.Adui huwa anasubiri wakati umelala(wakati ambao umetulia,hujui chochote kinachoendelea) ndipo wakati naye anakuja kupanda vya kwake. Neno linasema kuwa majani ya ngano yalipoanza kumea ndipo wakagundua kuwa kuna magugu pamoja nayo.Ngano haioti kwa siku moja,mpanzi alikuja kugundua kuna magugu baada ya muda kupita. Kumbuka adui alipanda magugu lakini hakusubiri yaote,alipomaliza kupanda akaondoka lakini madhara ya hiyo mbegu yalikuja kuonekana baada ya muda kupita.Ndio maana shetani anaweza kuzuia mwanamke kushika ujauzito toka akiwa mtoto mdogo lakini madhara ya hii mbegu inakuja kuonekana anapoingia kwenye ndoa na anapohitaji mtoto,hapa ndipo anakuja kugundua kuwa kuna ambacho sicho cha kiMungu kimepandwa. Ni vizuri sana kutafuta kujua kama kila kitu kipo sawa kwenye maisha yako,unaweza kuona kuwa hakuna tatizo kabisa kwenye maisha yako kwa sababu tu bado magugu hayajamea.Kaa vizuri na Mungu naye atakuonesha mahali penye pando ambalo silo lake na atalitoa. Katika ibada ya hii ambayo iliongozwa na Mtumishi wa Mungu Pastor Sunbella Kyando tulijifunza kuhusu namna adui ambavyo anatumia sana muda wa usiku kupanda uharibifu,na Jumatano ijayo tutakuwa na maombezi juu ya kuondoa kila pando ambalo silo la Mungu kwenye maisha yetu. UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HII : 0657 173 322 Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii Like our Facebook: https://www.facebook.com/Therealityof ... Follow our Instagram: https://www.instagram.com/realityofch ... Subscribe our YouTube: /channel/UC67L ... Also Subscribe Roc worshippers youtube channel:/channel/UCyVhAzjcFaJH7lxgiMQviGQ

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 43