المدة الزمنية 12:55

UWIANO WA HARAKA NA MATUMIZI YAKE KATIKA KUTAZAMA MADENI YA BIASHARA ZENYE HISA KATIKA SOKO LA HISA

بواسطة Emmanuel Matunda
171 مشاهدة
0
3
تم نشره في 2021/02/03

Viungo katika mitandao yetu ya jamii; https://www.instagram.com/matrich_investing/?hl=en https://www.facebook.com/Matrich-Investing-104068614639938/ https://twitter.com/MatrichInvesti1?s=09 MAELEZO KUHUSU UWIANO WA HARAKA Huu ni uwiano unaosaidia kupima uwezo wa kampuni katika kulipa madeni yake ya muda mfupi kwa kutumia rasilimali zenye ukwasi zaidi. Hivyo kampuni yenye uwiano wa haraka mkubwa huashiria ya kwamba kampuni hiyo inauwezo wa kulipa dhima zake za muda mfupi bila kuuza bidhaa zake au kupata ufadhili wa ziada kama vile mtaji au misaada ya kifedha Uwiano wa haraka unaonekana kuwa bora zaidi kuliko uwiano wa mtaji unaofanya kazi kwa sababu uwiano huu hautazami upande mmoja tu wa kuangalia kama biashara inathamani kubwa ya rasilimali za muda mfupi kuliko dhima za muda mfupi bali inaangalia pia kama biashara hiyo ina thamani kubwa ya rasilimali ambazo ni rahisi kubadili kuwa pesa au ambazo zipo katika mfumo wa pesa zitakazotumika katika kulipia dhima za muda mfupi katika muda huo Hivyo uwiano huu unalinganisha thamani ya rasilimali zenye ukwasi na thamani ya dhima za muda mfupi. Jibu la angalau 1 huashiria ya kuwa kuna ukwasi mzuri katika mfumo wa rasilimali ikija katika kuzitumia rasilimali hizi katika malipo ya dhima za muda mfupi MAHESABU YAKE 𝑹𝒂𝒔𝒊𝒍𝒊𝒎𝒂𝒍𝒊 𝒛𝒂 𝒎𝒖𝒅𝒂 𝒎𝒇𝒖𝒑𝒊 −𝑩𝒊𝒅𝒉𝒂𝒂 𝒏𝒂 𝑮𝒉𝒂𝒓𝒂𝒎𝒂 𝒛𝒊𝒍𝒊𝒛𝒐𝒍𝒊𝒑𝒊𝒘𝒂 𝒎𝒂𝒑𝒆𝒎𝒂/𝑫𝒉𝒊𝒎𝒂 𝒛𝒂 𝑴𝒖𝒅𝒂 𝑴𝒇𝒖𝒑𝒊

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 1