المدة الزمنية 11:44

DC KIMANTA AZIPONGEZA IDARA YA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI.

بواسطة MONDULI TV ONLINE
79 مشاهدة
0
0
تم نشره في 2020/06/12

DC KIMANTA AZIPONGEZA IDARA YA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI. Leo tarehe 11 Juni 2020 Mheshimiwa Iddi Kimanta Mkuu wa Wilaya ya Monduli amezipongeza idara ya Elimu Msingi chini ya Mkuu wa Idara Ndugu.Theresia Kyara akishirikia na Idara ya Elimu Sekondari kwa kuwezesha utoaji Elimu kwa waalimu wa Afya wa shule za msingi na Sekondari na mafisa Elimu Ngazi ya Idara,Waratibu elimu kata na walimu wakuu za shula za sekondari na msingi ili kupata mbinu watakazozitumia kufundisha wanafunzi pamoja na walimu wengine, ili kuweza kujikinga ugonjwa wa covid_19 . . . Dc Kimanta ameyasema hayo wakati anahitimisha kwa kufunga mafunzo hayo ya utoaji wa Elimu ya Utayari kwa walimu wa Afya na walimu wa shule za msingi na sekondari na Maafisa Elimu ngazi ya idara. Waliopata mafunzo ni Walimu Wakuu na Wakuu wa shule zote za serikali na zisizo za serikali, Maafisa Elimu Kata wote, Walimu wa Afya wa Kata zote msingi na Sekondari na maafisa ngazi ya idara. . . . Amewataka walimu kwenda kuchapa kazi kwani idara imeshajipanga kuhakikisha watakuwa salama na tendo la ujifunzaji liendelee kikamilifu. . . . Afisa Elimu Msingi Ndugu.Theresia Kyara amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Monduli kwa kuchangia kiasi cha shilingi Laki 3 kwa ajili kuunga mkono jitiada zinazofanywa na idara ya Elimu Msingi na Sekondari. Amemuomba Mh.Mkuu wa Wilaya kuendelea kuhamasisha wadau mbali mbali ili kupata vifaa vya kujilinda na na covid_19 kwa kila darasa kwa shule zote mara tuu shule zitakapofunguliwa. DC KIMANTA AZIPONGEZA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI. -IDARA YA ELIMU MSINGI -IDARA YA SEKONDARI Imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli🇹🇿 IDARA YA ELIMU MSINGI. 11JUNI 2020 ELIFURAHA RAPHAL(KABURU).

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 1