المدة الزمنية 43:37

Kutana na Kijana Mlemavu wa Viungo Mwenye Ndoto za Kuwa Rubani

بواسطة The Chanzo
304 مشاهدة
0
6
تم نشره في 2021/12/15

Wanasema usiache kuwa na ndoto haijalishi changamoto unazopitia. Pengine hakuna muumini mkubwa wa msemo kuliko Augustino Ilomo, kijana wa Kitanzania mwenye ulemavu wa kuongea na ambaye baadhi ya viungo vyake vya mwili havina uwezo wa kufanya kazi. Changamoto anazokabiliana nazo Agustino zingewashawishi watu wengi kukata tamaa na kuacha jitihada za kufanikisha ndoto zao za maisha. Hali haiko hivyo kwa kijana huyu ambaye licha ya changamoto hizo Agustino amefanikiwa kupata moja katika haki za msingi ambayo ni elimu chini ya usimamizi wa wazazi wake pamoja na wadau mbalimbali. Pamoja na changamoto hizo, Agustino ameweza kuhitimu masomo yake ya kidato cha nne huku akiwa na matumaini makuwa ya kufaulu na kuingia kidato cha tano. Hii ni simulizi ya maisha ya kijana huyo inayosimuliwa na wazazi wake pamoja na mwalimu wake. #TheChanzo

الفئة

عرض المزيد

تعليقات - 1