TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya, inamshikilia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyeregete iliyoko wilayani Mbarali, Adelhard Mjingo (44) kwa tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 14.